F Vita vya Ukraine: Msimamo wa Beijing juu ya vita unapingana na kanuni za China – Kamishna wa EU | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Vita vya Ukraine: Msimamo wa Beijing juu ya vita unapingana na kanuni za China – Kamishna wa EU

 


Msimamo wa China juu ya vita nchini Ukraine una athari mbaya kwa sura ya nchi, na kusita kwa Beijing kulaani uvamizi wa Urusi hubeba hatari kwa sifa, alisema Valdis Dombrovskis, Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Kamishna wa Biashara wa EU, ambaye anatembelea China.


"Uadilifu wa nchi daima umekuwa kanuni muhimu ya diplomasia ya kimataifa kwa China.


Vita vilivyoanzishwa na Urusi ni ukiukaji wa wazi wa kanuni hii, AFP inamnukuu Dombrovskis akisema huko Beijing. "China imekuwa ikisisitizia kila nchi kuwa huru kuchagua njia yake ya maendeleo."


"Kwa hivyo ni vigumu sana kwetu kuelewa msimamo wa China kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, kwa kuwa inakiuka kanuni za msingi za China yenyewe."


Mwezi Machi, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara rasmi nchini Urusi na kusema kuwa uhusiano kati ya Moscow na Beijing unaingia katika zama mpya. Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kufanya ziara nchini China mwezi Oktoba.

Post a Comment

0 Comments