Amend warudisha mafunzo ya usalama barabarani kwa bodaboda Dodoma


Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kufanyika mafunzo ya elimu ya Usalama barabarani kwa awamu ya kwanza katika Jiji la Dodoma hatimaye mradi huo wa kutoa elimu hiyo tunatarajia kuanza tena lengo likiwa kuwafikia madereva wengi wa bodaboda katika Jiji hilo.

Mafunzo hayo yanatolewa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushika na Ubalozi wa Uswisi nchini ambapo awali katika Jiji hilo la Dodoma madereva bodaboda 250 waliopatiwa mafunzo na sasa mradi huo umerejea tena baada ya kutolewa maombi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri kwamba ni vema mafunzo hayo yakatolewa tena.

 Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend, Amiri Matimba amewaambia waandishi wa habari kwamba mafunzo hayo  yataanza kutolewa leo Aprili 15, mwaka huu katika kata ambazo hazikupata mafunzo hayo yalipotolewa Februari mwaka huu.

Amefafanua mafunzo hayo yananalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki, abiria na watumiaji wengine wa barabara, hivyo kuzuia vifo na majeruhi wa matukio ya ajali ambapo wengi wao ni vijana.

Ameongeza kuwa Amend na Ubalozi wa Uswisi wamekubali ombi la mkuu wa wilaya ya Dodoma na kwamba mafunzo yanaanza rasmi April 15 mwaka huu na wadau mbalimbali watashiriki likiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Walimu wa Usalama Barabarani, Mwalimu Massava Ponera amewataka maofisa usafirishaji (bodaboda)kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli zao.

"Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yana umuhimu makubwa kwani mbali na vifo ajali za barabarani husababisha ulemavu wa kudumu huku takwimu za sensa nchini zikionesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na wengi wameamua kujikita katika ujasiriamali wa bodaboda.

Post a Comment

0 Comments