Na John Walter -Babati
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mheshimiwa Daniel Sillo, ametoa taarifa ya faraja kwa wananchi wa jimbo lake kuhusu maendeleo ya huduma za mawasiliano.
Kupitia kundi la WhatsApp ambalo anashirikiana na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, Mheshimiwa Sillo aliandika ujumbe akisema:
"Naomba niwajulishe kwamba kutokana na changamoto ya mawasiliano iliyokuwepo katika jimbo letu, tumefanikiwa kupata minara ya mawasiliano katika kata za Ufana, Secheda, Qameyu, Gidas, Qash, Nkaiti, na awamu ya pili inakuja kata ya Galapo, kijiji cha Ayamango."
Ujenzi wa minara hiyo unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakikabiliwa na matatizo ya mtandao.
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali za kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi wote, hata walioko vijijini.
Hii ni habari njema kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kuwa huduma hiyo itasaidia kuimarisha shughuli za kijamii na kiuchumi, hasa kwa vijana na wakulima wanaotegemea teknolojia ya mawasiliano katika shughuli zao za kila siku.
Hatua hii inaonesha dhamira ya serikali ya awamu ya sita ya kupeleka maendeleo kwa wananchi wote bila kujali maeneo yao ya kijiografia.
0 Comments