Na John Walter-Kondoa
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kondoa Mjini, Mariam Ditopile, amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa kura Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza leo mbele ya mgombea huyo wa urais wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kondoa, Ditopile alisema Rais Samia amefanya mambo makubwa ya maendeleo katika jimbo hilo na wananchi wanapaswa kumuunga mkono ili aendelee kutekeleza miradi zaidi.
"Rais Samia amefanya mengi Kondoa, kuanzia miradi ya afya, elimu, maji hadi barabara. Wanakondoa tunategemea mengi zaidi kutoka kwake, ndiyo maana tunapaswa kumuunga mkono kwa kura zetu," alisema Ditopile.

Aidha, aliahidi kwamba katika kampeni za uchaguzi huu atapita kila kona ya jimbo hilo kuhakikisha anawaomba wananchi kura za CCM, ili chama hicho kiendelee kushika dola na kusukuma maendeleo.
Ditopile pia aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha sauti ya Kondoa inasikika kupitia ushindi wa CCM.

0 Comments