F NCHIMBI AMTAKA KEMBAKI KUWA KAMPENA MENEJA WA ESTHER MATIKO WA JIMBO LA TARIME MJINI | Muungwana BLOG

NCHIMBI AMTAKA KEMBAKI KUWA KAMPENA MENEJA WA ESTHER MATIKO WA JIMBO LA TARIME MJINI



Na Timothy Itembe Tarime.

MGOMBEA mwenza wa Chama Cha mapinduzi DKT Emmanuel Nchimbi amemtaka aliyeongoza kura za maoni ya Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki kuwa kampena meneja wa aliyeteuliwa na Chama Cha mapinduzi,Esther Matiko.

Nchimbi alisema kuteuliwa Kwa Esther Matiko kugombea Jimbo la Tarime kupitia Chama Cha mapinduzi ni utaratibu wa CCM kupendekeza Mgombea na DKT Samia Suluhu Hassani amemwagiza kumtaka Michael Kembaki aliyeongoza kura za maoni  kuwa kampena Meja wa Mgombea aliyeteuliwa na Chama ili kuomba kura za Chama Cha mapinduzi ili kishinde Katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Okotoba 28, 2025.

DKT Nchimbi alitoa Kauli hiyo mjini Tarime Leo alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa Chama Cha mapinduzi nafasi ya Ubunge na Udiwani wanaotolana na Chama Cha mapinduzi ndani ya viwanja vya Chuo Cha uwalimu TTC ambapo alisema kufanya hivyo kutasaidia kuvunja makundi yaliyokiwepo.wakati wa kura za maoni ambapo alisema kuwa ili Chama kishinde lazima makundi yavunjwe na Chama kikishinda kitapata nafasi ya kuunda Dola.

Mgombea urais kupitia Chama Cha mapinduzi DKT Samia Suluhu Hassani ameahidi Siku 100 za mwanzo endapo atashinda uchaguzi na kuapishwa kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania ataanza na Bima ya Afya Kwa wote baada ya Kuna wagonjwa wengi wanahangaika na kuteseka kutibiwa pindi wanapo ugua wanakuwa hawana uwezo wa kumdu matibanu.

"Watu wengi wanashindwa kumdu matibanu pindi wanapo ugua kama DKT Samia Suluhu Hassani akifanikiwa kuwa Rais ameahidi kuanza na Bima ya Afya Kwa wote Kwa sababu Watu wanateseka na magonjwa na wengi hawamdi gharamaza matibanu pia 

Katika siku 100 za kwanza Nchimbi amesema Samia atatoa Ajira Kwa idara ya Afya na Katika kuimarisha Elimu Dr Samia atatoa Ajira 7000 Kwa Vijana ya walimu wa sayansi na pia tutaanzisha Gridi ya Taifa ya maji na ataenda kutoa shilingi Bilioni 200 Kwa wafanyabiashara"alisema Nchimbi.

Michael Kembaki alikiti kupokea maelekezo yaliyotolewa na mwenyekiti wake Taifa na Rais wa jamijuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassani ya kuwa meneja kampena wa Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko ili kuhakikisha Chama kinapata ushindi wa kishindo.

Kembaki alisema kwa miaka mitano chini ya serikali ya DKT Samia Suluhu Hassani mambo na miradi mingo imetekelezwa na kuwa hakuna Chama kingine chenye sera nzuri inayotekelezeka kama CCM.

Kembaki ambaye alikuwa Mbunge aliyemaliza mda wake alitumia nafasi hiyo kumkatibisha Mgombea mwenza wa Chama Cha mapinduzi,DKT Emmanuel Nchimbi Jimbo la Tarime ambapo alisema Watu wa Mara na Tarime wanakula kichuri karibu hapa tunakula kichuri"Ambapo Kembaki aliongeza kuwa nitaarifi Kwa Jimbo letu Tarime lipo salama na litaendelea kuwa salama ni.mpongeze Rais Samia ametoa shilingi Billion tisa Katika ujenzi wa soko kuu Tarime pia Watu wa Bugosi kulikuwa na mgogoro Watu hao wamelipwa"alisema Kembaki.

Kembaki alimaliza kusema amepokea Kwa mikono miwili uteuzi wa Rais kumteua kuwa meneja kampeni wa mteuliwa wa Chama Cha mapinduzi nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko na kuwa  kuteuliwa na Chama kuwa Mgombea wa CCM ni utaratibu wa kichama na kuomba waliokuwa nyuma yake kumuunga mkono  Esther Matiko ili kuhakikisha Chama kinapata ushindi wa kishindo.

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko alisema Moja ya kitu kilichomvutia kujiunga na Chama Cha mapinduzi na kuhama Chama chake Cha zamani Cha CHADEMA ni CCM kuwa na Fkra ya kuleta maendeleo Kwa watanzania

Matiko aliongeza kuwa miaka minne Hospitali ya kwangwa ambayo ujenzi wake ulianza miaka ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kwa awamu zote imekuja kukamilika ndani ya uongozi wa DKT Samia Suluhu Hassani pamoja na Hospitali ya Bomani imeboreshwa na kukarabatiwa na wananchi wanafrahia huduma.

Mgombea Ubunge huyo ameahidi kuwa akifanikiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini atahakikisha ananoresha miundombinu ya utalii na Kuboresha kiqanja Cha Ndege Cha magena kinaxhopokea watalii wengi ili kuendana na hadhi na kupongeza maboresho y

Post a Comment

0 Comments