Na John Walter -Babati
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Maryam Muhaj, amewaaga wachezaji 22 wanaokwenda kushiriki Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) jijini Mwanza, ambayo yatafanyika kwa siku 17 mfululizo.
Akizungumza wakati wa kuwaaga, Muhaj aliwapongeza kwa kuchaguliwa kuiwakilisha Manyara na kusisitiza kuwa wanapaswa kuibeba timu hiyo kama alama ya mkoa mzima.
Alisema michezo ni afya, inajenga undugu pamoja na mahusiano mazuri, hivyo wanapaswa kuitumia fursa hiyo kujitangaza vizuri na kuipa heshima Manyara.
"Kauli mbiu ya mwaka huu ni Michezo kwa watumishi kuongeza tija kazini, Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
Aidha, aliwataka wachezaji kushirikiana na kuonyana endapo mwenzao ataenda kinyume na maelekezo, huku akiwapongeza wakuu wa taasisi kwa kuwaruhusu watumishi kushiriki na kugharamia ushiriki wao katika michezo hiyo.
0 Comments