F TAKUKURU: Mapambano dhidi ya Rushwa ni ya jamii nzima | Muungwana BLOG

TAKUKURU: Mapambano dhidi ya Rushwa ni ya jamii nzima


TAASISI ya kupamba na rushwa TAKUKURU mkoa Tanga imeeleza kuwa mapambano dhidi ya Rushwa ni ya jamii nzima kwa ujumla ili kuhakikisha maendeleo hayarudi nyuma kwa utoaji na upokeaji rushwa.

Hayo yamebainishwa  na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga Ramadhan Nduwatah  wakati akifUngua warsha ya waandishi wa habari mkoa ambayo imelenga kuwapa mafunzo waandishi hususani kipindiki hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani  utakaofanyika Oktoba mwaka huu .

 Alisema kila mtu ajue elimu ya umuhimu wa thamani ya kura yake kwani kura ndio inayoweza kumpa mtu namna ya kumpata kiongozi atakayeweza kuleta maendeleo hivyo elimu ya thamani ya kura ya kila mtu ili katika mchakato wa kuwapata viongozi ambao ndio serikali.

Aidha alisema Takukuru imepewa majukumu ya kutoa elimu kwa kwa kila kundi kujua madhara ya rushwa katika jamii kuweza kufikia  malengo yake, maendeleo na haki kwani rushwa ndio advice wa haki.

Alisema mafunzo hayo ni mpango wa serikali kuweza kutoa elimu kwa wadau ili kujua madhara ya rushwa na miongoni mwa wadau ni pamoja na waandishi wa habari ili kipitia kalamu zao waweze kuwaelimimsha Jamii lakini kuibua hitendo vya Rymushwa.

Mafunzo hayo yaliweza kuhususha waandi shi wa habari wapatao takriba 50 lakini wameweza kuwafikia viongozi wa dini kwa umoja wao ili waweze kufikisha ujumbee huo kwa waumuni wao ili wapate kujua umuhimu wa kukataa Rushwa kwa maslahi mapana ya nchi na maendeleo.
misho.



 

Post a Comment

0 Comments