F Grace Mali aongoza Mahafali ya 17 shule ya msingi Masakta -Mbulu | Muungwana BLOG

Grace Mali aongoza Mahafali ya 17 shule ya msingi Masakta -Mbulu


Na John Walter-Mbulu
Mahafali ya 17 ya Shule ya Msingi Masakta, wilayani Mbulu, yamefana kwa heshima ya mgeni rasmi, Grace Mali, ambaye ni Mkurugenzi wa Grace Volleyball Club.

Akihutubia katika hafla hiyo, Bi. Mali aliwapongeza walimu kwa kazi kubwa ya malezi na ufundishaji kwa wanafunzi, akisema mchango wao ni nguzo muhimu ya mafanikio ya taifa. Pia aliwashukuru wazazi kwa kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema na dini, pamoja na kuwapa elimu ya kutambua na kupinga ukatili wa kijinsia.

“Nawaomba tuendelee kushirikiana katika kulea watoto wetu kwa maadili mema, maana wao ndiyo viongozi wa kesho. Elimu wanayoipata shuleni iambatane na malezi ya nyumbani,” alisema Bi. Mali.

Katika kuunga mkono jitihada za shule hiyo, mgeni rasmi alikabidhi vifaa vya michezo pamoja na mashine ya kuchapisha (printer), ili kuwezesha shughuli za kitaaluma na michezo shuleni hapo.

Uongozi wa shule, walimu na wazazi walimshukuru kwa moyo wa kujitolea na mchango wake, wakiahidi kutumia vifaa hivyo ipasavyo kwa maendeleo ya wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments