Na John Walter-Babati
Mahakama kuu Tanzania kanda ya Manyara chini ya jaji Nenelwa Mwihambi imeahirisha bila kupanga tarehe kesi iliyofunguliwa na CHADEMA dhidi ya msajili wa vyama vya siasa kupinga maamuzi yake ya kutowatambua viongozi walioteuliwa na baraza kuu januari 22, mwaka huu pamoja na kuzuia ruzuku kwa chama hicho.
kisi hiyo namba 23267/2025 imewakilishwa na mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili mkuu wa serikali Mark Mulwambo akisaidiwa na wakili Erigh Rumisha pamoja na wakili Nickson Tenges na mawakili upande wa chadema ni wakili Mpare Mpoki akisaidiwa na wakili Samwel Welwel pamoja na wakili Tadey Lister.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo mmoja wa mawakili wanaosimamia kesi hiyo wakili Tadey Lister amesema uamuzi huo umetolewa ili kupisha mahakama ya rufaa kutoa maamuzi ya rufaa iliyokatwa na upande wa serikali kupinga maamuzi madogo yaliyotolewa mahakamani hapo agost 28, 2025 na jaji wa mahakama hiyo Devotha Kamzora.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Chadema John Mnyika amesema kufuatia maamuzi yaliyotolewa oktoba 2,2025 na mahakama kuu kanda ya manyara maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa hayatotekelezwa na kufanyiwa kazi na anapaswa kuingiza katika akaunti ruzuku ya chama kuanzia alipositisha mpaka sasa.
0 Comments