F UWT mkoa wa Njombe waomba Wananchi wachague viongozi wanaotokana na CCM | Muungwana BLOG

UWT mkoa wa Njombe waomba Wananchi wachague viongozi wanaotokana na CCM

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe Aziza Kiduda ametoa wito kwa wanawake wilayani Makete kujitokeza na kuwapigia kura viongozi wa Chama cha Mapinduzi itakapofika Octoba 29

Amesema  mshikamano wa mafiga matatu – Rais, Mbunge na Diwani – ni msingi muhimu katika kusukuma maendeleo ya wananchi endapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuaminiwa kuongoza katika ngazi hizo.

Kiduda ameyasema hayo wakati wa ziara ya kamati ya Ushindi UWT mkoa wa Njombe walipokuwa  wilayani Makete, ambapo timu ya UWT mkoa wa Njombe imetembelea kata 23 kuanzia Oktoba 2, ambapo kamati hiyo  ina wajumbe 15 wanaozunguka kata zote za mkoa huo kwa lengo la kutafuta kura za CCM.

Amesema wananchi na wanachama wa CCM wanapaswa kuwa walinzi wa amani kwa kusimulia mazuri yanayotekelezwa na viongozi wa chama hicho, jambo litakalowasaidia kuendeleza mshikamano wa kisiasa na kijamii.

Aidha, Kiduda alisisitiza kuwa amani ni nguzo kuu ya maendeleo, hivyo wananchi wanapaswa kuithamini na kuitunza ili kila eneo liweze kufaidika na miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments