Maisha uliyonayo yanaweza yakawa mazuri sana ama mabaya kutokana na aina ya uchaguzi
unaofanya juu ya maisha yako kila siku. Mara nyingi uchaguzi tunaofanya katika
maisha yetu ndiyo huwa unaamua zaidi maisha yetu yaweje. Kama uchaguzi
unaofanya ni mbaya, ni wazi maisha yako yatakuwa mabaya na kama uchaguzi wako
ni mzuri basi maisha yako yatakuwa mazuri hivyohivyo hakuna atakayezuia hilo .
Kwa kuwa uchaguzi wowote tunaofanya katika maisha yetu
unakuwa una athari ni vizuri tukawa makini kidogo na uchaguzi wa mambo
tunayofanya kila siku. Nikiwa na maana kuwa inatakiwa tujue kama
kuna jambo tunalifanya ni muhimu kutambua lina athari zipi kwetu. Kama tumeamua kufanya kitu fulani tuanze kwa kutafakari
matokeo yake kwanza. Hivyo ndivo tunavyotakiwa kufanya ili kuwa na uchaguzi
sahihi katika maisha yetu.
Kwa uchaguzi sahihi tutazidi kufanya maisha yetu kuwa bora
siku hadi siku. Ikumbukwe pia kila kunapokucha tunanya aina nyingi sana za chaguzi ambazo
zinaamua hatima ya maisha yetu. Mara nyingi huwa ni watu wa kuchagua mavazi,
nguo za kuvaa, njia na mambo mengineyo mengi. Sasa ikiwa tunachagua mambo haya,
kwanini tusiwe na uchaguzi juu ya maisha yetu? Je, unajua ni aina gani ya
uchaguzi sahihi tunaotakiwa kuufanya katika maisha yetu ili kufanikiwa zaidi?
1. Chagua kuishi sasa.
Hii ndiyo siri ya wewe kuweza kufurahia maisha yako.
Hautaweza kufurahia maisha yako na kuyaona katika uzuri wake halisi ikiwa
unaishi kwa fikra sana
za siku ziliyopita ama siku za nyuma zaidi. Kwa kuishi kwako sasa, kuishi kwa
kutokuwa na hofu sana
juu ya kesho yako, hapo utakuwa unafanya uchaguzi sahihi utakao weza
kubadilisha maisha yako na kuwa ya furaha na yenye mafanikio kwako pia.
2. Chagua kuishi
maisha yasiyokuumiza.
Acha kuishi maisha ya kuumiza utaumia sana . Ili
kufanikwa kwa hili, jifunze kutokuyachukulia mambo kwa ujumla ili usiweze
kuumia zaidi. Ikiwa mtu atakwambia wewe ni mbaya, hufai hiyo yote inaweza ikawa
sawa kulingana na mtazamo wake. Hapo lakini wewe usije ukachukulia huo ndiyo
ukweli na kuanza kuumia na kujiona kweli hufai. Fuata ukweli ulio ndani yako
kuhusu wewe na siyo vinginevyo.
3. Chagua kuishi maisha ya ukarimu.
Haijalishi mtu amekufanyia nini katika maisha yako kitu
kikubwa cha kujifunza nikuwa mkarimu kwa wetu wengine. Unapokuwa mkarimu unakuwa
unaishi maisha ya utulivu ambayo mara nyingi yanakuwa hayana msuguano zaidina
wengine katika maisha yako. Kwa kuishi maisha hayo yatakusaidia kukupa furaha
na nguvu ya kufanikiwa. Hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi na kuwa hivyo.
4. Chagua kuishi kwa
kufanya mambo yako kwa uchache.
Ikiwa utajifunza kumudu tabia hii basi utaweza kuishi maisha
safi ya furaha
ambayo wewe mwenyewe utakuwa ni wazi unayafurahia kwa vyovyote vile iwavyo.
Jifunze katika maisha yako kuongea kidogo na kuwa msikilizaji sana . Jifunze pia kula chakula kiasi ili
kukujengea afya bora zaidi. Mambo mengi jaribu kuyafanya kwa kiasi hiyo itakuwa
ni siri mojawapo ya kuweza kukupeleka kwenye mafanikio.
5. Chagua kufanya mambo mapya.
Hautaweza kufanikiwa kama
utakuwa unafanya mambo yaleyale siku zote. Ili
kuweza kufanikiwa unalazimika kuchagua kufanya mambo mapya ambayo hujayazoea.
Katika kufanya mambo mapya ni lazima kujitoa mhanga na kukabiliana na kila aina
ya changamoto ili kuweza kufanikiwa, vinginevyo itakuwa ni ngumu sana kuweza kumudu kuleta
mafanikio tunayoyataka katika maisha yetu.
