Bilinganya imo katika
jamii ya mimea
inayohusisha nyanya, pilipili,
viazi mviringo na
nyanya mshumaa. Mboga
hii ina viini lishe
muhimu kama vile
madini aina ya
chokaa na chuma,
Vitamini A, B
na C, wanga,
protini na maji.
Mboga hii hutumika
kutengeneza supu au kama kiungo katika
vyakula mbalimbali.
Vilevile
huweza kuhifadhiwa kwa
kukatakata vipande na
kuwekwa kwenye makopo.
MAZINGIRA:
Zao hili
huhitaji hali ya
joto la wastani, udongo
wenye kina
kirefu na rutuba
ya kutosha na
usiotuamisha maji. Kwa
kawaida bilinganya hulimwa
zaidi ya msimu
mmoja, lakini katika
nchi za Kitropiki
(joto) zao hili
hulimwa kwa msimu
mmoja.
AINA:
Aina za bilinganya zinazolimwa
kwa wingi katika
nchi za ukanda
wa joto ni kama zifuatazo;-
1. Black Beauty:
Aina hii huzaa
sana , matunda
yake meusi, makubwa,
na ya mviringo
2. Florida Market.
Matunda ya Florida
Market yana umbo
la yai. Aina
hii pia huzaa
sana, lakini hushambuliwa
kwa urahisi na
ugonjwa wa mnyauko
bakiteria (Bacterial wilt)
3. Florida High
Bush.
Matunda yake ni
makubwa yenye umbo
la yai na
rangi ya kijani
kibichi iliyochanganyika na
nyeusi.
4. Newyork Spineless.
Matunda ya Newyork
Spineless ni ya
mviringo, makubwa na
yana rangi ya
ya zambarau.
5. Peredeniya.
Aina hii huzaa
sana, matunda yake
ni makubwa kiasi
na yana umbo
la yai.
Aina zingine za
bilinganya ni matale,
Kopek na Rosita. Aina hizi
huvumilia sana
mashambulizi ya ugonjwa
wa mnyauko bacteria.
KUOTESHA MBEGU:
Mbegu
huoteshwa kwanza kwenye
kitalu na baadaye
miche huhamishiwa shambani. Kabla
ya kusia mbegu,
tengeneza tuta lenye
upana wa mita
moja na urefu
wowote. Weka mbolea za
asili kama vile
samadi au takataka
zilizooza vizuri, kiasi
cha ndoo moja
au mbili katika
eneo la mita
mraba moja. Sia mbegu kiasi
cha gramu mbili
mpaka tatu (nusu
kijiko cha chai
chenye ujazo wa
gramu tano) katika
eneo hilo.
Gramu 500 za
mbegu zinatosha kupandikiza
katika eneo la
hekta moja. Nafasi
kati ya mstari
na mstari iwe
sentimeta 10 hadi
15 na kina
kiwe sentimita 1.5.
Baada ya kusia
mbegu fukia na
tandaza nyasi kavu
na kisha mwagilia
maji. Endelea kumwagilia kitalu
kila siku, asubuhi
na jioni, hadi
mbegu zitakapoota. Mbegu
huota baada ya
siku ya 10
hadi 12.
KUHAMISHA MICHE:
Miche huwa tayari
kwa kupandikizwa shambani baada
ya wiki sita
hadi nane. Wakati
huu huwa na urefu
wa sentimita 15
mpaka 20 (sawa
na urefu wa
kalamu ya risasi).
Mwezi mmoja kabla
kupanda miche, rutubisha udongo
kwa kuweka mbolea
za asili zilizooza
vizuri. Mbolea hizi
ni kama samadi,
mbolea vunde na
mbolea ya kuku.
Weka kiasi cha
tani 10 hadi
20 kwa hekta.
Kiasi hiki ni
sawa na kuweka
ndoo moja hadi
mbili zenye ujazo wa
lita 20 katika eneo
la mita mraba
moja. Mbolea ya
mchanganyiko aina ya
N.P.K yenye uwiano
wa 20:10:10 huwekwa
kwenye shimo wakati
wa kupandikiza mche.
Kiasi kinachohitajika ni
gramu tatu hadi
tano (sawa na
nusu kijiko mpaka
kijiko kimoja kidogo
cha chai) kwa
kila shimo.
Nafasi ya kupandikiza
hutegemea aina ya
bilinganya. Aina ndogo
hupandikizwa katika nafasi
ya sentimita 80
mpaka 100 kutoka mstari hadi
mstari na sentimita
50 mpaka 60
kutoka mche hadi
mche. Aina kubwa
hupandikizwa katika nafasi
nafasi ya sentimita
80 mpaka 100
kutoka mstari hadi
mstari na sentimita 80
mpaka 90 kutoka mche
hadi mche. Kazi
ya kuhamisha miche
ifanyike kwa uangalifu
mkubwa ili kuepuka
kuikata mizizi.
KUTUNZA SHAMBA:
1. Kuweka matandazo.
Mara baada ya
kupandikiza miche, tandaza
nyasi kavu. Matandazo
husaidia kuhifadhi unyevu,
huzuia magugu yasiote
na huongeza rutuba
ya udongo.
2. Palizi.
Hakikisha
shamba ni safi
wakati wote ili
kuzuia ushindani wa
chakula, maji na
mwanga kati ya
mimea na magugu.
Usafi wa shamba
pia huondoa maficho
ya wadudu waharibifu
na huzuia kuenea
kwa magonjwa.
3. Mbolea.
Mbolea ya kukuzia
aina ya S/A
huwekwa wiki tatu
baada ya mmea
kuanza kutoa maua . Kiasi
cha gramu tatu
hadi tano kuwekwa
kuzungukia kila mche.
Mbolea iwekwe katika
umbali wa sentimita
tano mpaka 15
kutoka kwenye shina,
hutegemea ukubwa wa
mche. Hakikisha mbolea
haigusi mmea.
4. Kukata kilele.
Wiki mbili baada
ya kupandikiza miche,
kata sehemu ya
juu ya mmea (kilele)
kama umepanda aina
ndefu ya bilinganya.
Hii itasaidia kupata
matawi matatu hadi
manne na mmea
kutengeneza kupata matawi
matatu hadi manne
na mmmea kutengeneza
umbile la kichaka.
Matawi yakizidi manne
yaondolewe ili kupata mazao
mengi na bora.
5. Kumwagilia.
Zao la bilinganya
hustawi vizuri likipata
maji ya kutosha.
Umwagiliaji ufanyike kila
siku asubuhi na
jioni kutegemea hali
ya hewa.
Kuzuia Wadudu Waharibifu
na Magonjwa.
Wadudu Waharibifu:
6. Vivyatomvu
wa Bilinganya (Eggplant
Lacebugs)
Wadudu hawa hushambulia zaidi
sehemu ya chini
ya jani. Hufyonza
utomvu wa majani na
kusababisha majani kuwa
na mabaka meupe
au njano. Mashambulizi yakizidi
majani huanguka chini.
Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa
kwa kunyunyizia moja
ya dawa zifuatazo;-
Deltamethrin
(Decis), Dimethoate (Sapa Dimethoate)
Fenvalerate (Sumicidin),
Lambda - Cyhalothrin (Karate).
7. Vidukari au wadudu
mafuta (Cotton Aphids)
Hawa ni wadudu
wadogo wenye rangi
nyeusi. Hushambulia majani
machanga na kuyasababisha kudumaa
na kukunjamana. Zuia
wadudu hawa kwa
kutumia mojawapo ya
dawa zifuatazo;-
Dimocron 50% E.C,
Lambda - Cyhalothrin (Karate) Dichlorvos (Nogos).
8. Utiriri wa Mimea
(Red Spider Mites).
Ni vidudu vidogo
vyenye rangi nyekundu
iliyoiva. Hushambulia
majani kwa kufyonza
utomvu. Majani yaliyoshambuliwa huonyesha
utando kama wa
buibui. Mashambulizi yakizidi
mea hudumaa, majani
hukauka na hatimaye
hufa.
Utiriri
unazuiwa kwa kutumia
dawa zifuatazo;- Acrex,
Karathane 25% W.P, Dimethoate,
Ekalux, Kelthane.
9. Minyoo Fundo (Root
knotnematodes).
Wadudu hawa hushambulia
mizizi. Hutoa kinyesi
ambacho ni sumu
kwa mmea. Sumu
hii husababisha mizizi
kuwa na nundu
kama ya mizizi
ya maharagwe. Mashambulizi yakizidi
mmea hudumaa, hunyauka
na hatimaye hufa.
Njia ya kuzuia
wadudu hawa ni
kubadilisha mazao kwa
mfano baada ya
kuvuna zao hili,
zao linalofuata lisiwe
la jamii moja
na bilinganya kama
vile nyanya, pilipili
na viazi mviringo. Pia
dawa aina ya
Carbofuran (Furadan) inaweza
kutumika.
Magonjwa:
1. Mnyauko
Bakteria ( Bacterial Wilt).
Ugonjwa huu husababishwa na
backteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka
ghafla hasa wakati
wa jua kali.
Mnyauko
bacteria unaweza kuziuwa
kwa kubadilisha mazao
shambani. Endapo ardhi
itashambuliwa na ugonjwa
huu zao la
bilinganya lisipandwe katika
eneo hilo kwa
muda wa miaka
mitatu hadi mitano.
Njia nyingine ni
kupanda aina za
bilinganya kama vile
Matale, Kopek na
Rosita ambazo huvumilia
mashambulizi ya ugonjwa
huu.
2. Phomopsis Vexans:
Ugonjwa huu husababishwa na
bacteria na kushambulia
majani, shina na
matunda.
3. Verticillium
Wilt.
Huenezwa na maji
na husababisha mmea
kudumaa, majani kukunjamana
na kuanguka.
Magonjwa ya Phomopsis
vexans na Verticillium Wilt
yanaweza kuzuiwa kwa
kung’oa ma kuchoma
moto mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha
mazao, na kuweka
shamba katika hali
ya usafi wakati
wote.
KUVUNA:
Bilinganya
huanza kutoa matunda
yaliyokomaa baada ya
miezi miwili hadi
mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji
huendelea kwa muda
wa zaidi ya
miezi minne na
hauna budi ufanyike
mapema mara matunda
yanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana
hayafai kulimwa kwa
sababu huwa na
kambakamba na mbegu
zilizokomaa.
Vuna mara mbili
au tatu kwa
wiki, kwa kutumia
kisu kikali ili
usiumize matunda.
MAVUNO:
Kwa kawaida zao
hili huzaa sana iwapo
limetunzwa vizuri. Shamba
lililotunzwa vizuri linaweza
kutoa mavuno tani
50 hadi 60
kwa hekta. Hata
hivyo mavuno mengi
hutegemea aina ya
bilinganya, umwagiliaji na
rutuba ya udongo.