Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa CCM wilaya Shinyanga mjini
Bw.Charles Sangulo wakati akitangaza rasmi matokeo ya kura za maoni jimboni
humo na kudai kuwa mchakato huo ulikuwa mkali uliojaa kashkash nyingi na vuta
nikuvute za hapa na pale lakini palipo na ushindani lazima apatikane mshindi
huku Mh.Steven Masele akiibuka mshindi na kuendelea kutetea jimbo la Shinyanga
mjini.
Nao baadhi ya wananchi wa jimbo la Shinyanga mjimi
hawakusita kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato
mzima katika kura za maoni na mabo yalikua kama
ifuatavyo.
Aidha baadhi ya wagombea wengine walioshindwa kupata nafasi
katika kinyanganyiro hicho wamelazimika kukubaliana na matokeo hayo kwa shingo
upande huku wakidai kuwa malalamiko yao
juu ya rushwa iliyokuwa imetawala katika kinyang'anyiro hicho yamekwama kwa
madai kuwa yamekosa ushahidi wa kutosha hali iliyosababisha kubadilika kwa hali
halisi ya matokeo hayo.
Na kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi kura za maoni CCM
kata ya Shinyanga mjini amemtangaza rasmi Bw.Gulam Hafiz Mukadama kuwa mshindi
wa kiti cha udiwani kwa kupata kura 182 dhidi ya mgombea mwengine katika
kinyang'anyiro hicho.
