Serikali ya UTURUKI imesema kuwa wapiganaji wa kikurdi
wamekamata vituo vya polisi vya nchi hiyo pamoja na kuua watu WATANO.
Wapiganaji hao wa kikurdi pia wamelipu bomu wafanyakazi wa reli katika vituo viwili
tofauti nchini UTURUKI.
Gavana wa jimbo la ADANA MUSTAFA BUYUK amesema wapiganaji wa
PKK wamelipua kituo cha polisi cha mjini
POZANTI, na kuua maofisa wa polisi.
Katika upande wa mashariki wa jimbo la KARS, wapiganaji wa
PKK wamelipua mabehewa na baadae kuwaua wafanyakazi wa reli ambao waliokuwa
wakifanyia marekebisho reli hiyo katika eneo la ADEM UNAL na kuua mfanyakazi
mmoja wa reli.
Ghasia kadhaa zimetokea nchini UTURUKI katika siku za hivi
karibu baada ya kikundi cha wapiganaji cha PKK kuhusishwa na vifo vya maafisa
wa polisi wa nchi hiyo katika mji wa SANLIURFA karibu kabisa na mpaka wa SYRIA .
Ghasia hizo zimesababisha serikali ya UTURUKI kutangaza
mapambano dhidi ya kikundi hicho cha PKK kaskazini mwa IRAQ .
Waziri mkuu wa UTURUKI AHMET DAVUTOGLU amesema mashambulizi
dhidi ya kikundi cha wapiganaji hao wa PKK hayataisha hadi pale wapinagaji hao
wa PKK watakaposhusha chini mikono yao .
