Alikiba adai album yake Cinderella iliuza kopi milioni 2

Hitmaker wa Chekecha Cheketua, Alikiba amesema album yake ya kwanza, Cinderella ilivunja rekodi na kuuza ‘double platinum’ (nakala milioni mbili).

Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Alikiba alisema mpaka leo hajasikia kama rekodi hiyo imevunjwa.

“Kiukweli album yangu ya kwanza ya Cinderella ndio ilivunja rekodi na sijasikia mpaka leo kama rekodi hiyo imevunjwa,” alisema. “Sijui (nakala) ni milioni mbili vile, kitu kama hicho, kila album ilikuwa inauzwa mia mbili,” alisema Alikiba.

Pamoja na kuingiza takriban shilingi milioni 200 kupitia album hiyo, Kiba alisema utoto ulikuwa mwingi.

“Utoto mwingi, nilijenga kupitia album, vitu vingi nilifanya, yaani mpunga nilikuwa ninao halafu sijui kama ninao. Wewe unafikiri mimi nilipumzika bure,” aliongeza muimbaji huyo.



Mpya zaidi Nzee zaidi