Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP, Ernest Mangu amefanyia ziara katika mitambo ya kuchakata na kusafirisha gesi iliyopo madimba mkoani Mtwara na kupongeza juhudi za ulinzi zinazofanywa na shirika la Maendeleo ya Petroli nchini TPDC.
Katika ziara hiyo, IGP Mangu alitembezwa katika visima vya gesi, na mitambo hiyo na kujionea hali ya ulinzi katika visima na mitambo ya kuchakata gesi na kuipongeza TPDC, kushirikisha ulinzi shirikishi wa wananchi na kampuni ya SUMA JKT, mbali ya jeshi la polisi.
IGP Mangu ameongeza jeshi lake litaangalia kwa namna gani litaongeza nguvu ziadi katika ulinzi wa miundombinu hiyo muhimu kwa taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk, Joseph Mataragio, amesema ziara ya mkuu wa huyo wa jeshi la polisi ni nafasi nzuri kwao ili kujiona wapo katika nafasi gani kiulinzi wa miundombinu hiyo na kupokea ushauri wa kuboresha zaidi ulinzi wa Miundombinu hiyo.
Awali IGP mangu alipata taarifa za uendeshaji na ulinzi wa Visima na Miundombinu ya kuchakata gesi, kutoka kwa watendaji wa kampuni tanzu ya TPDC ya GASCO.
Katika ziara hiyo IGP Mangu alipata fursa ya kupita katika vituo vyote vinavyopokea gesi kutoka Madimba mkoani Mtwara mpaka Kinyerezi jijini Dar es salaam.