Kijiji cha Igula wamelalamikia uwepo wa tatizo la wazee

WANANCHI katika kijiji cha Igula wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa wamelalamikia uwepo wa tatizo la wazee, watoto chini ya umri wa miaka 5 na wanawake wajawazito kutozwa pesa ili kupata huduma za afya na matibabu katika kituo cha afya kijijini hapo jambo ambalo wamesema ni kinyume na sera ya afya.

Wakizungumza ktk mkutano wa wazi uliofanyika kijijini hapo kwa lengo kuona changamoto zilizopo ktk sekta ya afya wananchi hao wamesema inawashangaza kuona bado wazee, watoto na wakina mama wajawazito wanatozwa pesa wakati wanapohitaji huduma za afya na matibabu.

Bi Koga Mihama ambaye ni Mratibu wa mradi wa kudai uwajibikaji na utawala bora ktk sekta ya afya ambao unaendeshwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la TACOSODE chini ya ufadhili wa shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID) anasema upatikanaji wa taarifa ni muhimu na ndio njia pekee ya kuwajengea uwezo wananchi.
Mpya zaidi Nzee zaidi