Serikali kufuta sheria zinazokandamiza wanawake

Naibu waziri wa fedha na mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema serikali itaendelea kufuta sheria za kibaguzi zinazomkandamiza mwanamke kwa lengo la kumlinda dhidi ya vitendo vya ukatili.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo wakati akifungua mkutano wa wanawake wa uwiano wa kijinsia ulioandaliwa na taasisi ya wanawake wemye mafanikio TWAA Dkt. Kijaji amesema serikali pia itaweka sheria mpya pale ambapo hakuna sheria na ni kwenye maeneo muhimu.
Dkt.Kijaji amesisitiza wanawake kupewa kipaumbele na kusisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika maeneo mengi ikiwemo katika kazi.
Ameongeza kuwa Suala la jinsia lina wachangiaji wengi ambao wanatoa michango tofauti katika harakati za maendeleo lna kuwataja watendaji wakuu kuwa ni pamoja na serikali sekta binafsi na wadau wa maendeleo.
Mpya zaidi Nzee zaidi