Wabunge walalamika kutokutekelezwa Agizo la Waziri Geita

MBUNGE wa jimbo la Geita Constantine Kanyasu na mbunge wa viti maalumu kupia chadema  Mkoa wa Geita  Upendo Peneza kwa pamoja wameshangazwa na kitendo cha Mgodi wa wa dhahabu wa GGM kushindwa kutekeleza agizo walilopewa  na Naibu waziri wa nishati na madini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wandishi wa Habari  mara baada ya ya kutembelea eneo hilo liloko  katika mtaa wa katoma kata ya Kalangalala Wilaya na Mkoa wa Geita  na  kukuta hakuna kitu chochote kilichofanyika tangu agizo litolewe na Naibu waziri wakati wa ziara yake Mkoani humo.

Wabunge hao wamesema wanashangazwa kuona agizo la Naibu waziri wa nishati na  madini la kuziba mtaro wa majia  linapuuzwa na viongozi wa Serikali ya Wilaya na Mkoa  wakikaa  kimywa kana kwamba hawakuwepo kwenye ziara hiyo.

Akijibu malalamiko hayo kaimu Afisa madini Mkoa wa Geita amesema Agizo la Naibu waziri halijapuuzwa na kwamba amekwisha kuandikia Barua GGM juu ya utekelezaji huo huku Meneja mahusiano ya jamii wa mgodi huo Manase Ndoroma akisema wanalifanyia kazi.

Febuari 24  Naibu waziri  wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliupa mgodi wa GGM siku tatu wawe wamekamilisha kujenga tuta la kuzui maji kutoka katika milima ya mgodi huo kuingia kwenye makazi ya watu jambo ambalo mpaka sasa limegonga mwamba.
Mpya zaidi Nzee zaidi