Mapambano dhidi ya dawa za kulevya Mkuu wa Wilaya ya Muheza aomba ushirikiano kwa wananchi

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuwafichua wanaojihusisha na uuzaji usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Wito huo ameutoa wakati akihutubia wananchi wa katika hafla ya uzinduzi wa visima viwili vya maji katika kata ya Bwembwera na kijiji cha kwakifua wilayani muheza .

Amesema vita dhidi ya dawa za kulevya itafanikiwa endapo wananchi watashiriki na kutoa taarifa za kuwafichua wahalifu na kwamba endapo jirani yako atabainika kujihusisha na wewe ukashindwa kutoa taarifa utakua umeshiriki kutenda kosa.

Akizungumza katika uzinduzi huo mbunge wa jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu amesema kukamilika kwa mradi huo kumefikisha idadi ya visima 18 katika kipindi cha mwaka mmoja na kupunguza kero ya maji kwa wananchi.

Balozi Adadi amesema pamoja na uchimbaji wa visima hivyo serikali imetoa shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kuchukua maji kutoka Pongwe wilayani Tanga hadi muheza .
Mpya zaidi Nzee zaidi