Shirika la kimataifa la utafiti wa kugushi,rushwa na uchunguzi-CFRI-Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya wataalam wa kugushi-ACFE-wameipongeza serikali ya Tanzania katika mapambanao ya dhidi ya ufisadi na rushwa na kuwataka watanzania kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kujenga maadili kwa watumishi wa umma.
Wakizungumza na waandishi wa habari,kiongozi wa CFRI Tanzania Bwana Gebla Mahoo amesema dhamira ya serikali inalenga kuvuta dhana iliyojengeka kuwa swala la mtu kushika mamlaka furani ni fursa ya kutajirika na kuziomba baadhi ya asasi za kirai zinazolalamikia swala la uvunjaji wa sheria, kutambua swala la ukiukwaji wa maadili kuliko ukiukwaji wa sheria ambao kimsingi adhabu zake zimeshaainishwa.
Mkuu wa utawala,ushirikiano wa maendeleo wa mfuko wa maendeleo serikali ya Finland-FLCS- Bibi Clarah Ruhara amesema katika kusaidia mapambano dhidi ya rushwa na na ufisadi hapa nchini,serikali ya Finland imetoa zaidi ya euro elfu 58 kwa cfri ili kuwezesha utekelezaji wa mradi wa mwaka mmoja kuwajenge uelewa wananchi katika ngazi ya chini kuhusu rushwa,ufisadi katika maeneo ya Rungwe, Ngara,Hai, Bukombe na Mtwara.