Mtoto wa Bondia Mohammed Ali alivyozuiliwa Kuingia Marekani


Mtoto wa bigwa wa bondia wa kÅŸmataifa kutoka Marekani Mohammed Ali azuiliwa katika uwanja wa ndege kutokana na jina lake nchini Marekani.

Mtoto huyo anayetambulika kwa jina la Mohammed Ali Jr mwenye umri wa miaka 44 alihojiwa kwa muda wa masaa mawili alipokuwa akirudi kutoka safarini akiwa na mama yake mzazi Bi Khalilah Camacho Ali aliyekuwa mke wa Mohammed Ali.


Jr akishirikiana na mama yake alikuwa akitokea nchini Jamaica ambapo alienda huko mnamo mwezi Februari.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani Mohammed Jr alizuiliwa kutoka na jina lake kuwa chimbuko la kiarabu.

Mohammed Jr na mama yake walizuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Fort Lauderdale mwezi Februari.
Mpya zaidi Nzee zaidi