Mwanariadha afariki ghafla baada ya kumaliza mbio Kilimanjaro


Mwanariadha Mkenya, Charles Maroa(36) amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla baada ya kumaliza mbio katika Mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Jumapili tarehe 26 Februari.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polis Mkoa wa Kilimanjaro, Willbroad Mutafungwa, mwanariadha huyo alipoanguka, alipewa msaada wa kuwahishwa Hospitali ya KCMC lakini alipofikishwa hospitalini hapo madaktari walibaini kuwa alishafariki.

Mkenya huyo alikuwa akishiriki mbio za Kilomita 21 katika mbio hizo zilizoshirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kimataifa na kushuhudia Mtanzania, Emmanuel Giniki, akifanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza.
Mpya zaidi Nzee zaidi