Watu watatu wameuawa akiwemo Mkuu wa upelelezi

Watu watatu wameuawa akiwemo Mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Kibiti, mgambo mmoja , pamoja na mtumishi wa ofisi ya maliasili ya kijiji cha Jaribu Mpakani Kata ya Mjawa Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, kufuatia mabigano ya risasi yaliyofanyika usiku wa jana majira ya saa mbili kati ya Jeshi la Polisi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi ambapo baada ya tukio hilo kufanyika magaidi hao waliamuru wananchi wachukue mali ukiwemo mkaa, zilikuwepo kwenye ofisi ya Maliasili na baadae kuichoma moto ofisi hiyo.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea maeneo ambayo tukio hilo lilitokea, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema serikali haifurahishwi na matukio ya kuuawa kwa rai wake ambao hawana hatia, hivyo ametoa siku tatu kwa wakazi wa kijiji hicho kutoa ushirikiano kwa jeshi la poli ili kuweza kuwabaini wahusika wa tukio hilo na hatimae wachukuliwe hatua za kisheria.

Nchemba amesema kuwa tukio hilo la mauaji linafanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia kumi katika maeneo ya Mkoa wa Pwani ambayo ni Kibiti, Mkuranga , na Jaribu ambapo kufikia hatua hiyo Serikali inataraji kuunda kikosi kazi maaluum kwajiili ya Mkoa Pwani kitakachokuwa kikipambana na magaidi huku akitoa onyo kwa wananchi ambao wanaficha magaidi wanaofanya matukio ya uhalifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo amsema ni jambo la kusikitisha kwa jamii ya watanzania kuona tukio la mauaji linafanyika huku wananchi wakishuhudia na kuchukua mali ambapo amesema kufuatia kufanyika kwa tukio hilo kama mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama atahakikisha anasimamia usalama wa wananchi wa eneo hilo unapatikana, huku akitoa mapenedekezo ya kusitisha safari za madereva wa pikipiki maalufu kama bodaboda kuanzia majira ya saa kumi na mbili jioni kwani kwa kiasi kikubwa pikipiki zimekuwa zikitumika kwenye matukio ya uhalifu, huku mbunge wa Mkuranga Ally Ungando akielezea hali ya wasiwasi iliyotawala kwa wananchi wake kufuatia kufanyika matukio ya mauaji.
Mpya zaidi Nzee zaidi