Hata ningekuwa na haki ya kushtaki, nisingemshtaki Diamond- Saida Kalori


Kupitia kipindi cha TakeOne kinachorushwa na CloudsTv Saida Karoli anasema yeye alikuwa haelewi masuala ya mikataba. Hivyo alijikuta mikataba ilionyesha kwamba haki za malipo ya nyimbo zake zilikuwa kwa meneja wake. Mfano, alipofuatilia malipo baada ya Diamondplatnumz na Rayvanny kurudia wimbo wake #Salome, alikuta kwamba aliyekuwa meneja wake ameshalipwa na yeye akaja kuambulia pesa kidogo tu ( ' pesa ya soda ' )

Lakini SaidaKaroli anasema yeye wimbo huo ni kama aliutoa bure kwa Diamondplatnumz na anamshukuru sana kwani kitendo cha Diamond kurudia wimbo huo kimekuwa na faida kwake.


"Hata ningekuwa na haki ya kushtaki, nisingemshtaki @diamondplatnumz. Mimi ni kama nilikuwa nimekufa na aliporudia huo wimbo nimefufuka. Hivyo kwa moyo mmoja......nisingeweza kumshatki na ninamshukuru." - #SaidaKaroli. .
.
Mpya zaidi Nzee zaidi