Mvua Kubwa yasababisha Nyumba 124 zilizopo katika kata za Pugu na Buyuni kuezuliwa mapaa

Nyumba 124 zilizopo katika kata za Pugu na Buyuni katika manispaa ya Ilala jijini Dsm zimeezuliwa mapaa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kuambapatana na Upepo mkali majira ya saa tisa mchana jana katika maeneo hayo.

Aidha madarasa manne katika shule ya msingi Kigogo fresh nayo yameezuliwa mapaa na kusababisha nyufa katika madarasa mengine nane huku watoto wawili wakijeruhiwa kufuatia mvua hiyo iliyoambatana na Upepo mkali.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na katibu tawala wa manispaa ya Ilala walitembelea maeneo hayo kujionea hali halisi ilivyokuwa.

Aidha katika maeneo ya Zavala,Pugu station mkuu huyo wa wilaya alijionea nyumba nyingi zikiwa zimeezuliwa mapaa huku wakazi wa nyumba hizo wakiwa katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma yao.
Mpya zaidi Nzee zaidi