Tundu Lissu: Polisi walionikamata walikataa kuniambia kosa langu


Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amekamatwa na polisi katika mahakama ya Kisutu wakati akitoka kuhudhuria kesi yake ya uchochezi.

Taarifa ya kukamatwa lwa Lissu imethibitishwa na Afisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ambaye amesema kuwa Lissu amekamatwa bila kupewa maelezo yoyote ya sababu za kukamatwa kwake, na amepelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam..

Kupitia mitandao ya kijamii, Lissu ameandika....

"Nimekamatiwa mahakamani Kisutu mara tu baada ya waendesha mashtaka wa serikali hii kunifutia kesi iliyotokana na kukamatwa kwangu bungeni Dodoma mwezi uliopita.

Hiyo kesi wameifuta kwa maelezo kwamba serikali haina nia tena ya kuendelea na kesi hiyo. Sikutoka hata nje ya mahakama nikakamatwa tena. Wamenileta Central kwa mahojiano.

Mapolisi walionikamata wamekataa kuniambia wananikamata kwa kosa gani. Kwa hiyo sijui kosa nilofanya hadi sasa. Nadhani sababu ina uhusiano wa moja kwa moja Uchaguzi wa Rais wa TLS unaofanyika wiki ijayo."



 
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..

Mpya zaidi Nzee zaidi