Sanchez aitosa Arsenal, atimkia Juventus


Tetesi zinasema Alexis Sanchez amekataa mikataba yote iliyoletwa mbele yake na rsenal.Mazungumzo bado yanaendelea lakini ni wazi Sanchez anaweza akaondoka Arsenal kama anachotaka itafikiwa.Baada ya hali ya sintofahamu kati ya Arsenal na Sanchez kutokea,tayari timu zishaanza kupiga hodi kwenye kambi yake kutafuta saini yake.Wachina wapo,Chelsea wapo lakini Juventus wanaonekana wako serious zaidi.

Gazeti la nchini Italia liitwalo Carreiro Del Sport linasema £28m zinampeleka Sanchez kwenda Juventus mwishoni mwa msimu huu.Fabio Guildi na Guissepe Morata mabosi wa Juventus wanamtaka Sanchez pamoja na kiungo wa Lyon Corentin Tollisso,Juventus wanawataka waje wote kwa pamoja katika dirisha kubwa lijalo la usajili.Hii sio mara ya kwanza kwa Juventus kumtaka kwani walijaribu kumchukua kabla hata ya Arsenal,mwaka 2011 kabla Sanchez hajaenda Barcelon,Juventus walijaribu kumchukua kutoka Udinesse.

Sanchez anataka Arsenal wampe £250,000 kwa wiki hela ambayo ni wazi kwamba inaonekana ni ngumu kwa Arsenal kumpa kiasi hicho.Kama Sanchez ataondoka Arsenal litakuwa pigo kubwa sana kwao,tayari ana magoli 20 katika michexo 34 aliyoichezea Arsenal na kuondoka kwake ni wazi kutaiathiri Arsenal haswa katika eneo lao la ushambuliaji.

Tayari Arsenal wameshaanza mazungumzo na wachezaji mbali mbali ili kuziba pengo la Sanchez kama akiondoka.Marco Reus yupo kwenye orodha ya wanaotakwa na Arsenal,lakini pia Alexendre Lacazzete naye yumo.Arsenal walijaribu kumchukua Lacazzete toka msimu uliopita lakini ikashindikana,msimu huu wanaonekana watarudi kwa nguvu mpya.Lacazzete ana magoli 27 msimu huu,huku akifunga 103 katika misimu yake mitatu iliyopita.



Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote, Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ... 

Chakufanya ni Kubofya Link hapo chini na Ufate Maelekezo ya Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako... USIWE NA WASIWASI HUDUMA HII NI SALAMA KABISA..


Mpya zaidi Nzee zaidi