Kichapo cha magoli 5-1 kwenye uwanja wa Emirates walichotoa Bayern Munich kwa Arsenal ndio habari ya ‘mujini’ kwenye kurasa za habari za michezo za magazeti mengi ya England.
Kila gazeti limeipa uzito habari hiyo ambayo imeitikisa dunia hasa matokeo ya jumla (aggregate) kuwa Bayern Munich 10-2 Arsenal.
Arsenal imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza England kuondoshwa kwenye michuano ya UEFA Champions League kwa kichapo kikubwa zaidi.




