Zlatan amekubali adhabu ya kufungiwa mechi tatu baada ya kumpiga kiwiko Tyrone

Mshambuliajia wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic, ameamua kukubali adhabu iliyotolewa dhidi yake na chama cha soka England FA, kufungiwa kucheza mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko beki wa AFC Bournemouth Tyrone Mings.

Zlatan alitenda kosa hilo wakati wa mchezo wa Jumamosi ya March 4  2017  kati ya Man United dhidi ya AFC Bournemouth, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Old Trafford na kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, Zlatan sasa atakosa mchezo wa robo fainali ya FA Cup vs Chelsea na mechi za EPL za Middlesbrough ana West Brom.
Mpya zaidi Nzee zaidi