Wakati Tanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki zikipambana na biashara ya pembe za faru, Mahakama ya katiba ya Afrika kusini imelipinga jaribio la serikali la kutaka kuweka marufuku kwa biashara ya pembe za faru katika matumizi ya ndani.
Watunzaji wa wanyama pori hao wamedai kuwa, kuruhusu biashara hiyo kuendelea kufanyika kihalali kutaweza kupunguza idadi ya faru wanaouwawa kutokana na kwamba pembe za faru zinaweza kukatwa na kuacha wanyama hao hai.
Hata hivyo wahifadhi wa wanyama pori hawakubaliani na hatua hiyo.
