MWENYEKITI WA KAMATI HIYO, HAWA GHASIA.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imesema Bunge linakabiliwa na madeni makubwa yaliyosababishwa na kutopatikana kwa fedha za kutosha wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.
Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imeishauri serikali kuhakikisha inamalizia kupeleka kwenye Mfuko wa Bunge bakaa ya bajeti ya matumizi mengineyo Sh. bilioni 8.3 ya mwaka 2016/17.
Kamati hiyo pia imeshauri serikali kuridhia maombi ya Bunge ya bajeti ya nyongeza ya Sh. bilioni 21.196 ili liweze kutekeleza majukumu yake ya kikatiba kwa kipindi kilichobaki kufikia Juni 30, mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia, aliyasema hayo bungeni mjini hapa juzi alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2016/17 pamoja na makadirio ya fedha kwa mwaka 2017/18.
Ghasia alisema kamati imeelezwa kuwa bakaa hiyo ya Sh. bilioni 8.3 haitatosha kutekeleza shughuli zilizobaki katika kipindi cha Aprili hadi Juni, mwaka huu, hivyo inaishauri serikali kuridhia maombi ya bajeti hiyo ya nyongeza.
“Mfuko wa Bunge umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya kutopokea kwa wakati mgawo wa fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na wakati mwingine kupokea fedha pungufu kulinganishwa na ilivyoombwa na kuidhinishwa,” alisema.
Ghasia alisema kamati yake inaishauri serikali kuhakikisha inazingatia maelekezo ya kifungu cha 48 cha sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 kinachoitaka Hazina kutoa fedha kwenye Mfuko wa Bunge kwa kila robo mwaka.
Alisema kamati yake pia inaishauri serikali ihakikishe inatoa fedha zinazohitajika kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati na Bunge ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa shughuli husika.
Kamati hiyo pia iliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuzingatia sheria katika kushughulikia mgogoro wa uongozi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF).
HOTUBA YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisoma hotuba ya makadirio ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/18, alisema ofisi yake inaomba kuidhinishiwa Sh. bilioni 121.65 kwa ajili ya Bunge kati yake, Sh. bilioni 114.45 zikiwa za matumizi ya kawaida na Sh. bilioni 7.2 za matumizi ya maendeleo.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake, inaomba kuidhinisha Sh. bilioni 171.66. Kati yake, Sh. bilioni 74.64 ni za matumizi ya kawaida na Sh. bilioni 97.02 za matumizi ya maendeleo.
Akizungumzia utekelezaji wa bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2016/17 na mipango ya mwaka 2017/18, pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu alisema hadi kufikia Machi mwaka huu, jumla ya ajira 418,501 zimezalishwa nchini.
Kati yake, 239,017 sawa na asilimia 57 zimezalishwa katika sekta binafsi wakati 179,484, sawa na asilimia 43, zimezalishwa kutokana na shughuli za sekta ya umma ikiwamo miradi ya maendeleo.
Waziri Mkuu alibainisha mambo sita ambayo yanapaswa kuzingatiwa ambayo ni ustawi wa nchi kwa kudumisha amani na utulivu, kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi kwa hiari pamoja na kufichua wakwepa kodi, uzingatiaji wa misingi ya afya bora, matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa manufaa ya kizazi kijacho, kuongeza nidhamu na uwajibikaji, na kupiga vita biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
Katika hotuba hiyo, Waziri Mkuu pia alieleza mambo mbalimbali yaliyofanywa na serikali kwa mwaka huu wa fedha katika sekta za maendeleo zikiwamo kilimo, maliasili na utalii, viwanda, mifugo, madini, nishati, ujenzi, usafirishaji, mawasiliano, elimu, maji, afya, habari na michezo ambayo aliimwagia sifa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na mwanariadha Alphonce Simbu kwa kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.