England.MESUT Ozil amefichua kwamba moja ya sababu zinazomfanya asuesue kutoa uamuzi kuhusu dili jipya la kubaki Arsenal ni kutokana na kushindwa kuelewa hatima ya Arsene Wenger.
Kiungo huyo Mjerumani alisema amekuwa na uhusiano mzuri na Wenger, kocha ambaye amekuwa akimtetea kutokana na kelele za mashabiki, ikija akaondoka, basi kila kitu kitatibuka.
Ozil anaogopa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki kwenye timu hiyo kisha ikafika mwisho wa msimu Wenger akaondoka na kuja kocha wmingine.
Kocha, Wenger mkataba wake utafika tamati mwisho wa msimu huu na hajabainisha wazi kwamba ataendelea kubaki kwenye timu hiyo ya kuonyesha dalili hizo. Ozil anataka uhakika kama hajasaini dili jipya.
Wenger amekuwa kocha wa Arsenal kwa zaidi ya miaka 20, lakini siku za karibuni mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakipiga kelele wakimtaka asisaini mkataba mpya baada ya timu yao kuchapwa na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kushindwa kuonyesha upinzani kwenye Ligi Kuu England.
Ozil alisema Wenger alikuwa sababu moja ya kumfanya ajiunge na Arsenal wakati alipotokea Real Madrid, hivyo kwa sasa anasubiri kufahamu hatima ya Mfaransa huyo.
"Si muhimu tu kwangu mimi, bali kwa klabu nzima,"alisema Ozil na kuongeza. “Ni muhimu kufahamu kama anabaki au anaondoka. Tunahitaji kufikiria hilo tukielekea msimu ujao.
"Yeye ni muhimu sana. Katika maisha yangu ya soka nimekuwa nikifanya uamuzi si kwa sababu ya klabu bali ni kwa sababu ya makocha pia. Ukiwa mchezaji ni muhimu sana kuwa na kocha anayekuamini na anayeweza kukufanya ukue.
"Nilipoondoka Madrid kuja Arsenal,nilifanya hivyo kwa sababu aliniambia nitakuwa chaguo lake la kwanza. Ni hivyo tu na bado tunaelewana hadi leo."