Wahamiaji haramu 15 raia wa Ethiopia wakamatwa Momba

Jeshi la polisi na idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 15 raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafiri kwenda  Afrika Kusini ambapo wamekutwa wakiwa wamefichwa kwenye shamba la mahindi katika kijiji cha Ipumpila  wilayani Momba mkoani Songwe.

Wananchi wa kata ya Ndalambo ndio waliobaini kuwepo kwa wahamiaji haramu.

Afisa uhamiaji mkoa wa Songwe Elizeus  Mshongi amesema  tukio hilo linatokea wakati ambapo tayari raia wengine watano wa Ethiopia wameshakamatwa wakahukumiwa ,na kwamba  changamoto kubwa iliyopo ni wahamiaji haramu hao kusaidiwa na watanzania wanaojua njia za  maficho na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani jumatatu hii kukabiliana na mkono wa sheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia