Na. Ahmad Mmow.
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa zisizo lipiwa ushuru zenye thamani ya shilingi 70.33 milioni katika mamlaka ya mji wa Kilwa Kivinje. Hayo yalielezwa jana mjini Kilwa Masoko, na kaimu meneja wa TRA wa mkoa wa Lindi, Masawa Masatu kwenye taarifa mfupi aliyomsomea mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai. Kuhusu bidhaa hizo zilizokamatwa. Masatu alisema bidhaa hizo zilizokamatwa usiku tarehe 31 mwezi uliopita, katika bandari bubu ya Gombawana iliyopo katika kijiji cha Mnago kata ya Kivinje - Singino zinathamani ya shilingi 70, 331, 000/=.
Wakati thamani ya kodi iliyopaswa kulipiwa bidhaa hizo ni shilingi 16, 900, 000 /=. Kaimu meneja huyo aliitaja bidhaa iliyokamatwa kuwa ni madumu 1327 ya mafuta ya kupikia yenye ujazo wa lita ishirini kila moja. "Baada ya kupata taarifa tulikwenda eneo la tukio, kwa bahati mzuri majira ya saa mbili usiku tulifanikiwa kuyakuta mafuta hayo aina ya Mikogoldi (MICO GOLD) na Vikingi (VICKING) yaliyotengenezwa katika nchi za Malaysia na Indonesia yakiwa yametelekezwa kwenye vichaka ambayo yalishushwa katika bandari hiyo bubu, "alisema Masatu.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai. Alisema miongoni mwa changamoto kubwa zilizopo katika wilaya hiyo ni wingi wa bandari bubu, ambazo zinatumika kuingiza na kutoa bidhaa za magendo katika wilaya hiyo. Akibainisha kwamba ukubwa wa eneo la bahari na vifaa vichache vya doria kunachangia uwepo wa bandari hizo. Alisema juhudi kubwa zinahitajika katika kukabiliana na tatizo hilo na njia pekee ni viongozi na wananchi kushirikiana katika vita hiyo.
Alisema bandari bubu licha ya kutumika kushishia na kupakilia bidhaa za magendo lakini pia ni chanzo cha uharibifu wa mazingira yaliyopo maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi. Kwasababu ili kupata barabara ya kufika baharini nilazima ifyekwe mikoko. Kuhusu madhara ya magendo katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya alisema wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa wilaya zenye rasilimali nyingi zinazotokana na maliasili zilizopo wilayani humo.
Ingeweza kuwa ni miongoni mwa wilaya zenye uchumi mkubwa. Hata hivyo kukosekana kwa uzimamizi thabiti na utunzaji sahihi wa maliasili hizo kunaifanya iwe ni miongoni mwa wilaya masikini. "Maliasili zilizopo zikisimamiwa na kulindwa vema hata halmashauri ya wilaya ingengeweza kujiendesha yenyewe bila kutegemea serikali kuu.
Inasikitisha kuona inakatiwa umeme kwasababu ya kushindwa kulipa bili wakati mbao zenye thamani ya mamilioni ya shilingi zinatoroshwa, "alisema Ngubiagai.Alisema tatizo kubwa lililopo ni wananchi wengi na baadhi ya viongozi wakuchaguliwa kutotoa ushirikiano na serikali kuwafichua wanaofanya biashara za magendo na wanaofanya uvuvi haramu. Badala yake baadhi ya viongozi wanashirikiana na kuwalinda wahalifu."Tunamshukuru mkuu wetu wa mkoa kwakuanzisha kikosi kazi maalumu cha kupambana na wahujumu uchumi wa aina hiyo .
Nasisi tumejipanga mtu akijiona alifanikiwa siku moja asidhani kila siku alifanikiwa hatatoka wala kuingia salama na bidhaa za magendo, "alisisitiza Ngubiagai. Aliongeza kusema bidhaa za magendo zinasababisha wafanyabiashara halali kushindwa kumudu kukabili ushindani wa soko. Kwasababu bidhaa zilizoingizwa kwa njia haramu zinauzwa bei rahisi kuliko za wafanya biashara wanaotimiza na kutekeleza matakwa ya kisheria.
Kwahiyo wanakata tamaa na kuacha kufanya biashara na kusababisha serikali kukosa mapato yanayotokana na kodi ya mapato na tuzo nyingine zilizopo kisheria. Hadi sasa mwenye mafuta hayo ambayo yameingia katika wilaya hiyo bila kulipiwa ushuru hajapatikana.