Upinzani wapinga uteuzi wa waziri mkuu DR Congo

Muungano mkuu wa upinzani unaoongozwa na Felix Tshisekedi mtoto wa aliyekuwa upande wa upinzani Etienne Tshisekedi , umeomba jumuia za kimataifa kuitisha mazungmzo tena kati ya wanasiasa na kanisa katoliki nchini DRC baada ya kusitishwa .

Muungano huo unapinga kuteuliwa kwa waziri mkuu ambae siyo chaguo lao jambo wanalosema linakiuka makubalino yalifanywa Dec baina ya serikali na upinzani .

Uteuzi huo wa waziri mkuu umeugawanya Zaidi upinzani huku upande mmoja sasa ukidai Rais kabila ndiye kizuizi cha juhudi za kutafuta amani ya kudumu nchini humo , Hii ni taarifa ya Mbelechi Msoshi
Mpya zaidi Nzee zaidi