Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetanabaisha kuwa wameanza kufuatilia vyanzo vya mapato vya Msanii nyota wa Muziki wa Bongo Flavar Nasib Abduli ( Diamond Platnum) ili kumpangia kodi Stahiki anayopaswa kulipa.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, amesema kuwa TRA inazungumza na Diamond kuhusu nyanzo vyake vya mapato .
“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo''.amesema Kayombo.
