Nchini India katika jimbo la Telangana, jimbo ambalo linapatikana katikati mwa nchini nyuzi joto imeripotiwa kupita kipimo cha 46.
Vyombo vya habari nchini India vimefahamisha kuwa joto kali liliokumba jimbo hilo tangu mwanzoni mwa April limesababisha vifo vya watu zaidi ya 160.
Jarida la Hindustan Times limetangaza kuwa nyuzi joto zaidi ya 40 imesababisha maafa nchini.
Idara ya hali ya hewa imetangaza kuwa hali hiyo ya joto kali itaendelea hadi juma lijalo.
