Singida United yazidi kujiimarisha

Miraj Adam akipokea jezi namba 4 ya Singida United.

Kikosi cha Singida United FC kimezidi kujiimarisha kwaajili ya maandalizi ya michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara baada ya kumsajili beki Miraji Adam kwa mkataba wa miaka miwili.

Singida United ni kati ya timu tatu zinazodhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Miraji amesajiliwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho kinachonolewa na Hans van der Pluijm, beki huyo aliyeanza kupata uzoefu akiwa na Simba, alimaliza msimu uliopita akiitumikia African Lyon ambayo imeshuka daraja.
Mpya zaidi Nzee zaidi