Nyota wa Rnb kutoka Tanzania, Ben Pol anayetamba na ngoma yake 'Tatu' aliyomshirikisha rapa Darassa amesema anadalili zote ya kuwa msanii wa kimataifa baada ya kupata ofa na kolabo nyingi na wasanii wa nje.
Msanii wa Rnb, Ben Pol
Ben pol amezungunza hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Bongo Flava Top20 kinachoruka East Africa Radio na kuongeza kuwa ngoma yake inayofuata amefanya na msanii Chidimna wa Nigeria na ipo tayari, itakuwa ni kolabo yake ya pili na msanii mkubwa wa Afrika baada ya ngoma yake "Phone" aliyomshirikisha Mr. Eazi kutoka Ghana.
Mbali na hilo Ben Pol amedokeza kufanya ngoma nyingine na msanii mkubwa kutoka Marekani Trey Songz.
"Nina kolabo nyingi zinakuja, nimeshafanya moja na Chidinma wa Nigeria ipo tayari, pia nina ofa ya ngoma 10 kutoka kwa 'director' wa msanii Trey Songz wa Marekani ambapo nitaweza kufanya kazi moja na Trey Songz" - amesema Ben pol
Aida msanii huyo amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kuachia albam yake yenye nyimbo 6 maarufu kama E.P.
