Matokeo ya wali yameonesha Chama tawala cha Angola MPLA kimeibuka mshindi wa uchaguzi wa wabunge.Chama hicho kimepata asilimia 61 ya kura zilizopigwa siku ya Jumatano, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha UNITA kilichopata asilimia 27 kimepinga matokeo hayo, ambapo uchaguzi huo unakamilisha utawala wa rais Jose Eduardo Dos Santos.
Uchaguzi huo unakamilika leo kutokana na kucheleweshwa kusambazwa kwa makaratasi ya kupigia kura katika zaidi ya vituo kumi vilivyopo maeneo ya vijijini. Hata hivyo chama tawala cha MPLA kimechukua uongozi mkubwa wa zaidi ya asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa.
Ushindi wa MPLA unamaanisha kwamba urais unakabidhiwa kwa aliyekuwa waziri wa ulinzi Joao Lourenco ambaye aliteuliwa kuwa mrithi wa Dos Santos.