Mufti Kuu asema "Tumepoteza Dira"


 Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry bin Ally amekiri kuwa dhehebu la kiislamu kwasasa limepoteza dira kwa kile alichadai kumekuwa na masheikh wacahache kwa uelewa wao wamekuwa wakiamini wako sahihi kumbe wanaupotosha umma.
Mufti Abubakary Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa  kongamano la siku mbili lenye lengo la kuwaeleza Walinganiaji, Makhatib na maimamu umuhimu wakuilewa itikadi sahihi ya usilamu ili kuwafahamisha waislamu itikadi hiyo waweze kuondokana na makundi ambayo yanasambaza itikadi potofu katika jamii juu ya uislamu na kusababisha utengano na uvujnifu wa amani.

Aidha Mufti Abubakary amehimiza maimamu na masheikh watangaze itikadi sahihi juu ya uislamu ili waumini wa dini hiyo wasijiingize katika uvunjifu wa amani
Kwamujibu wa mratibu wa Kongamano hilo Sheikh Mbwana Ahmadi Urari, amesema kongamano limeandaliwa na People of Charity ambapo limekusanya washiriki 60 wakiwemo maimamu na wahubiri wa dini hiyo katika Jiji la Dar es salaam
Mpya zaidi Nzee zaidi