Na Ahmad Mmow, Lindi.
MAKOMO wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kitendo cha kuchelewa kusambazwa na kutolewa pembejeo za kilimo kwa wakulima na kusababisha baadhi ya wakulima wa korosho kushindwa kupata kwa wakati.
Makamo wa Rais alionesha masikitiko hayo alipokuwa anafunga maenesho ya 24 ya wakulima (Nane nane) katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi. Samia alisema amepata taarifa kuwa mwezi Mei mwaka huu wakulima wa korosho walihaidiwa na serikali kuwa wangepewa bure dawa aina ya salfa. Ambapo hadi sasa kiasi kilichosambazwa na kutolewa ni tani 14000 Kati ya tani 18000 zilizohaidiwa. Huku tani 4000 zikiwa zipo bandarini.
Alisema anazo taarifa kuwa hadi mwezi Juni mwaka huu kunabaadhi ya wakulima walikuwa bado hawajapta pembejeo. Ikiwamo dawa hiyo inayopemdwa na kutumiwa na wakulima wengi wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Akibainisha pia anazo taarifa kuwa dawa hiyo inauzwa kwa bei ya shilingi 80, 000 kwa kila mfuko mmoja. Kiwango alichokisema ni kikubwa kikilinganishwa na bei ya ya awali ya shilingi 15, 000.
Kufuatia hali hiyo makamo huyo wa Rais amemtaka waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo, Dkt Charles Tizeba ahakikishe kuwa wizara yake pamoja na halmashauri zihakikishe mfumo wa usambazaji na utolewaji pembejeo unaboreshwa. Lengo likiwa ni kutoruhudu makosa yaliyofanyika yatokee tena.
Makamo wa Rais Samia, ambae anatambulika kwa hulka ya upole alisema kama yaliyotokea yalisababishwa na utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa serikali katika ugawaji wa pembejeo hiyo ya aina ya salfa, waziri Tizeba awashugulikie watendaji hao na apelekewe taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo haraka ofisini kwake na yasitokee tena
"Namimi nawahakikishia (wananchi) nitambana kwa yote aliyohaidi. Na niseme katika hili sitakuwa Samia yule mnaye mjua, "Samia alisisitiza agizo lake.
Aliongeza kusema anafahamu korosho kwa msimu wa 2016 /2017 ziliingizia serikali fedha nyingi za kigeni. Hivyo hawezi kuruhusu uzembe wa aina yoyote utakao sababisha soko la zao hilo na mengine kushuka. Mbali na hayo makamo wa Rais alitumia hadhara hiyo kuwatoa hofu wazabuni wanaoidai serikali. Kwamba imekamilisha uhakiki wa madeni ya wazabuni hao wa pembejeo.
"Ila niseme hali sio mzuri, najana natumai mmemsikia Rais akisema kuna pembejeo hewa zifikazo bilioni 38. " Waziri wa fedha upo hapa, nichikue fursa hii kukuagiza kuwasilisha taarifa ya uhakiki huo kwenye vyombo vya uchunguzi, "alisema Samia.
Makamo wa Rais pia alizungumzia mtindo mbinu, ikiwamo ya barabara na bandari katika kuhakikisha mazao yanasarishwa kwa wakati kutoka mkoa wa Lindi. Alisema kwa sasa inatumika bandari ya Dar-es-Salaam kusafirishia korosho. Kwakuwa meli kubwa na zakati haziwezi kutia nanga katika bandari ya Lindi. Hata hivyo mkandarasi amekamilisha ujenzi wa karavati 10 za boksi, zenye urefu wa mita 46,ambayo ni sawa na asilimia 48 ya kazi yote. Ambapo kwa upande wa barabara alisema tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Masasi-Nachingwea hadi Ruangwa kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 91 umefanyika.
Aliongeza kusema kwamba nyaraka za zabuni zimeshwasilishwa kwa Wakala wa barabara (TANROADS). Maenesho ya wakulima kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi, kwa miaka minne mfululizo. Ambapo mwaka huu ni wa mwisho kufanyika katika viwanja hivyo kitaifa.