Majeruhi wa Chapecoense wapigwa 5-0 na Barcelona

Mchezaji Alan Ruschel amecheza mechi yake ya kwanza tangu anusurike kwenye ajali iliyoua watu 71 mwaka jana.

Mechi hiyo ya kumbukumbu ilizikutanisha Chapecoense na Barcelona, mchezo ulioisha kwa wababe wa Hispania kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 huku mabao hayo yakifungwa na Lionel Messi, Luis Suarez, Sergio Busquets, Gerard Deulofeu na Denis Suarez.

Ndege iliyopata ajali ilikuwa imewabeba wachezaji na wafanyakazi wa klabu, huku kati ya watu 77 waliokuwamo ni sita pekee walinusurika.
Mpya zaidi Nzee zaidi