Waziri Tizeba: Sitaki vikwazo usafirishaji Chakula

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dk Charles Tizeba amefunguka na kutoa tamko kuwa hivi sasa ni ruksa kwa mkulima yoyote kusafirisha chakula kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine wowote ndani ya Tanzania.

Waziri Tizeba amesema hayo leo kwenye kilele cha sherehe ya siku ya Wakulima Nane Nane ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Lindi na kutaka watu wanaoweka vikwazo vya kibiashara hususani chakula au mazao kutoka sehemu moja kwenda nyingine waache mara moja.

"Mfanyabiashara asikutane na vikwazo vyovyote kuuza mazao yake ndani ya Tanzania, tunataka biashara ndani ya nchi isiwe na vikwazo, wapo watu wameanza kufanya vikwazo, hatuwezi kuendesha nchi kwa namna hii, naomba wananchi waachwe wapeleke mazao yao au chakula kuuza sehemu ambayo wao wanaitaji kuuza ndani ya nchi hii" alisisitiza Waziri Tizeba
Aidha Waziri Tizeba amewataka wakulima kutouza chakula chote ambacho wamekipata bali wanatakiwa kuhifadhi chakula cha kutosha ndani na kama wanaauza basi wanatakiwa kuuza ziada ya chakula ambacho kimepatikana, ila wanapaswa kuuza ndani ya nchi tu na si vinginevyo.

Makamu wa Rais Mama Samia pia alisisitiza kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara au mkulima kutozwa ushuru zaidi ya mara moja na kudai kwa mazao yanayozidi tani moja mkulima au mfanyabiashara anayesafirisha chakula au mazao akishalipa kwenye halmashauri moja hatakiwi kulipa tena ushuru wowote sehemu yoyote ambayo atapeleka mazao hayo au chakula hicho.
Mpya zaidi Nzee zaidi