Msuva ashindwa kujiunga na Taifa Stars,nafasi yake yachukuliwa na kiungo wa Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye anayechezea klabu ya Difaa El Jadida ya nchi ya Morocco ameshindwa kujiunga na kikosi cha Taifa Stars baada ya kutokuwa na kibali kinachomruhusu kutoka nchini Morrocco.

Hayo yamewekwa wazi na Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga baada ya kuwasiliana na nyota huyo na kusema nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mwingine kutoka klabu ya Yanga ambaye ni Kiugo Emmanuel Martin.

"Simon Msuva ameshindwa kuja kujiunga na wenzake kutokana na kutokuwa na kibali kirefu cha kuingia na kutoka nchini humo 'visa' ambacho kinamnyima haki ya kutoka mara kwa mara japokuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco limeanza kufanya jitihada za  kumfanikishia kupata kibali cha muda mrefu ili iwe rahisi kwa mchezaji kutoka na kuingia kama anahitaji katika timu ya taifa", alisema Mayanga.

Pamoja na hayo, Mayanga amesema "mpaka sasa nyota wengine wote wameripoti Taifa Stars wakiwamo wale wa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo", alisema Mayanga.

Kwa upande mwingine, Mayanga amesema wachezaji wengine waliyowasali  wapo kambini Jijini Dar es Salaam wakiendelea kujifua kuelekea mpambano huo wa kirafiki.
Mpya zaidi Nzee zaidi