Wapinzani 12 waliotuhumiwa kumkashifu rais Kabila waachwa huru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wapinzani hao 12 walikamatwa katika maandamano dhidi ya rais Kabila yaliofanyika Desemba 19 mwaka 2016.
Waandamanaji hao waliandamana wakimtaka rais Kabila kuondoka madarakani.
Mahakama ya Kivu-Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewaacha huru wapinzani hao.
Maandamano hayo yalifanyika wakati ambapo muhula wa rais Kabila ulikuwa umefikia ukingoni.
Miongoni mwa wapinzani waliokamatwa na kuachwa huru alikuemo mwanamke mmoja.