Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imetoa siku saba kwa wavamizi waliovamia na kuharibu zaidi ya kilometa za mraba elfu moja za kitalu cha uwindaji cha Katoto kutokana na shughuli za kibinadamu kuondoka ili kunusuru kitalu hicho kinachotegemewa kwa uwindaji wa kitalii lakini kikiwa kimetembelewa na watalii wawili tu mwaka huu.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Marko Gaguti ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe ametoa maagizo hayo baada ya kuongoza kamati ya ulinzi na usalama kutembelea eneo hilo,na kubaini uwepo wa mifugo na shughuli za kilimo kinyume cha sheria katika eneo hilo la msitu wa makere na uvinza.
Afisa wanyamapori wa wilaya ya Kasulu Mohamed Omari amesema uvamizi huo umepunguza idadi ya watalii wanaofika kwa ajili ya uwindaji katika kitalu hicho ambacho awali kilikuwa na wanyama na viumbe wengi waliowavutia watalii na kuiingizia nchi mapato.