Watatu wauawa katika shambulizi Marekani

Taarifa kutoka idara ya usalama ya mji wa Thornton zinasema kuwa watu watatu wamepoteza maisha katika  shambulizi lililofanyika katika  duka moja Colorado nchini Marekani.

Kupitia mtandao wa Twitter Polisi imesema kuwa leo Alhamisi wanaume wawili na mwanamke mmoja wameuawa kwenye duka la Walmart la mjini Thornton.

Wanaume hao wawili wameuawa katika eneo la tukio hilo wakati mwanamke nae amefariki kutoka na majeraha wakati akifikishwa hospitali.

Polisi imeripoti kuwa mshukiwa amekimbia na operesheni ya kumsaka imeanzishwa.

Msemaji wa Polisi Victor Avilla ametaka watu kuwa mbali na eneo la tukio hilo.

Shambulizi hili limefanyika siku mbili baada ya shambulizi la kigaidi la mjini New York na bado haijafahamika kuwa shambulizi la Colorado lina uhusiano wa kigaidi au laa.
Mpya zaidi Nzee zaidi