Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza wajibu wa watanzania wote kuelekeza mawazo yao katika kutunza mazingira ili kuyarejesha katika hali ya kawaida badala ya kuziachia baadhi ya taasisi ambapo amesema shughuli za kiinadamu zimekuwa sababu ya uharibifu wa mazingira katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Mama Samia ameyasema hayo jijini dar er es salaam muda mfupi kabla ya kukagua mradi wa ujenzi wa ukuta katika ufukwe wa bahari maeneo ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni ambapo kutokana na uharibifu wa mazingira baadhi ya mikoa ikiwemo iliyokuwa ikisifika kwa baridi sasa inaelekea kurandana na mikoa ya Pwani ambayo inasifika kwa joto.
Amesema athari zote zinazotokea katika kipindi hiki zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, mvua kunyesha zaidi ya kiwango na kusababisha mafuriko.
Naye Waziri wa nchi muungano na mazingira January Makamba amesema licha ya kuwa Tanzania haichangii katika uzalishaji wa hewa ukaa inayosababisha uchafuzi wa mazingira na kuathiri nchi nyingine duniani bado imekuwa ikishiriki kwa kikubwa katika kukabiliana na mabadiliko hayo ambapo sasa inatakeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kuta katika fukwe za bahari unaotekelezwa katika maeneo matatu dsm, Pangani na Zanzibar lengo likiwa kuzuia ardhi asiendelee kuliwa na bahari.
Jumla ya dola milioni 5.8 zimetolewa na mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi ambapo kati ya hizo zimetumika dola milion 5.5 kwa ajili ya ukuta wa kigamboni na ocean Road barabara ya Barack Obama huku dola laki 9 zikitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mitaro katika maeneo ya Ilala Malapa na Mtoni kwa Azizi Ally.